KUJITANGAZIA UHURU
Kujitangazia
uhuru kutoka katika utumwa wa kiroho, kuwatangazia nduguzako uhuru
kutoka katika utumwa wa kiroho ni kazi inayohitaji kusimama kwako
mwenyewe na kujitambua.
Ezekiel 37:3 BWANA MUNGU alimwambia
Ezekieli "Mwanadamu, je mifupa hii yaweza kuishi?" Ezekiel akamjibu
"BWANA MUNGU wajua wewe"
Ezekiel 37:4 akamwambia "Toa unabii juu ya mifupa hii uiambie enyi mifupa mikavu lisikie neno la BWANA"
Ezekiel 37:5 BWANA MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya "Tazama nitatia pumzi ndani yenu nanyi mutaishi.
Kama
BWANA MUNGU alivyomwambia Ezekieli, na wewe ni Ezekieli wa familia
yako, biashara yako, mashamba yako, ndoto zako na nchi yako. Tabiri kwa
yale unayotaka yatokee ondoa ukaufu, tabiri uzima.
Ondoa kushindwa, tabiri ushindi ndipo utayaona mafanikio makubwa.
Ezekiel
37:11 Kisha akamwambia Ezekieli "Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba
yote ya Israeli, tazama wao husema mifupa yetu imekauka, matumaini yetu
yametupotea, tumekatiliwa mbali kabisa.
Ezekieli
37:12-13 BWANA MUNGU akamwambia ezekieli "Basi tabiri uwaambie BWANA
MUNGU asema hivi, tazama nitafunua makaburi yenu na kuwapandisha kutoka
katika makaburi yenu enyi watu wangu, nami nitawaingiza katika nchi
yenu.
Kuna ushindi baada ya kuwekwa huru, kuna kutawala
baada ya kuwekwa huru, kuna umiliki baada ya kuwekwa huru, kuna amani
baada ya kuwekwa huru.
Chukua hatua leo ukajitangazie uhuru wako na ubarikiwe na BWANA kwa kujitangazia uhuru wako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni