HALELUYA MWANA WA MUNGU
SOMO LA LEO: usemi wa mwanadamu.
usemi
wa mwanadamu ni uwezo wa mwanadamu wenye nguvu zaidi. kwa sababu kwa
manenoyake anaweza kuleta manufaa makubwa. lakini pia anaweza kuleta
hasara kubwa katika neno la MUNGU bibilia inasema katika (MITHALI 12:18)
kuna anenaye bila kufikili, kama kuchoma kwa upanga bali ulimi wa
mwenye haki ni afya
Matatizo mengi uliyo nayo katika
maisha yako, ndoa, biashala,kazini, shambani, na katika jamii anayo
kuzunguka. yanasababishwa na matumizi mabaya ya usemi wako unawakwaza
watu kwa usemi wako,
(MITHALI 10;19) katika wingi wa
maneno hapakosi kuwa na maovu baliu yeye azuiaye midomo yake hufanya
akili, tunza mdomo wako kwa usalama wako mwenyewe, Wasifu wa mtu sio
mavazi tu bali hutemea maneno ya kinywa chako mwenyewe
Mpumbavu
na mwenye hekima wakinyamaza huwezi kuwatambua mpumbavu ni yupi na
mwenye hekima ni yupi, utawatambua tu wakianza kujieleza ndipo
atajulikana mpumbavu na mwenye hekima, jitaidi sana kufikili kabla
haujasema usije ukaonekana mpumbavu machoni pa watu,
hiki
ndicho kipimo cha utu wako na heshima yako mbele ya wanao kutazama, ni
aibu kwa mtu mwenye utashi na ukwasi kutamka hadhalani maneno yasiyo faa
mbele ya jamii
BWANA YESU AKUBALIKI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni