BWANA WETU YESU ASIFIWE
SOMO LA LEO: Kuwa kiungo katika mwili wa christo yesu
ukristo sio dini bali usiano na bwana wetu yesu. kwa yesu wetu hakuna
dini. na watu hawaendi mbinguni kwa tiketi ya madhehe yao, hutaingia
mbinguni kwa upentecoste au uassembles wako.
Ndugu
yangu. kuwa na majina makubwa ya madhehebu hakukusaidii kitu. Bali
kinacho saidia ni ushirika wako na bwana wetu yesu. neno la BWANA
linasema hivi katika kitabu cha WAEESO5;29-30 maana hakuna mtu
anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama kristo
naye anavyolitendea kanisa.sio dhehebu wala dini.
kwa
kuwa tu viungo vya mwili wake. yani kristo. kwanini leo kuna kutengana
baina ya madhehebu, sote tu viungo vya mwili wake yesu,mbinguni
tutaingia kwa utakatifu tu wala sii vinginevyo bwana akusaidie uponyeke
imani yako
kumbuka kuwa sehemu ya mwili kuna faida tano
1. KUPENDWA hakuna mtu alie wai kuchukia kiungo cha mwili wake mwenyewe .unapendwa na yesu kwa sababu uu kiungo cha mwili wake
2.KULINDWA hakuna mtu asie linda viungo vyo mwili wake. kristo naye utulinda
3.KUWEZESHWA hakuna asie viwezesha viungo vya mwili wake, una wezeshwa na yesu kwasababu uu sehemu ya mwili wake yani kanisa
4.KULISHWA. unalishwa na yesu kwasababu wewe ni sehemu ya nwili wake (kanisa)
5.KUJALIWA. hakuna asie ujali mwili wake bali uulisha na kuutunza kama yesu anavyo litendea kanisa lake hapa Duniani
UBARIKIWE NA BWANA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni