Jumapili, 12 Mei 2013

BWANA WETU YESU ASIFIWE

   SOMO LA LEO: Kuwa  kiungo katika mwili wa christo yesu


  ukristo sio dini bali usiano na bwana wetu yesu. kwa yesu wetu hakuna dini. na watu hawaendi mbinguni kwa tiketi ya  madhehe yao, hutaingia mbinguni kwa upentecoste au uassembles wako.

Ndugu yangu. kuwa na majina makubwa ya madhehebu hakukusaidii kitu. Bali kinacho saidia ni ushirika wako na bwana wetu yesu.  neno  la BWANA linasema hivi katika kitabu cha WAEESO5;29-30 maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama kristo naye anavyolitendea kanisa.sio dhehebu wala dini.

kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. yani kristo. kwanini leo kuna kutengana baina ya madhehebu, sote tu viungo vya mwili wake yesu,mbinguni tutaingia kwa utakatifu tu wala sii vinginevyo bwana akusaidie uponyeke imani yako


kumbuka kuwa sehemu ya mwili  kuna faida tano

1. KUPENDWA hakuna mtu alie wai kuchukia kiungo cha mwili wake mwenyewe .unapendwa na yesu kwa sababu uu kiungo cha mwili wake
2.KULINDWA hakuna mtu asie linda viungo vyo mwili wake. kristo naye utulinda
3.KUWEZESHWA hakuna asie viwezesha viungo vya mwili wake, una wezeshwa na yesu kwasababu uu sehemu ya mwili wake yani kanisa
4.KULISHWA. unalishwa na yesu kwasababu wewe ni sehemu ya nwili wake (kanisa)
5.KUJALIWA. hakuna asie ujali mwili wake bali uulisha na kuutunza kama yesu anavyo litendea kanisa lake hapa Duniani


                                         UBARIKIWE NA BWANA
                HALELUYA MWANA WA MUNGU



   SOMO LA LEO: usemi wa mwanadamu.

 usemi wa mwanadamu ni uwezo wa mwanadamu wenye nguvu zaidi. kwa sababu kwa manenoyake anaweza kuleta manufaa makubwa. lakini pia anaweza kuleta hasara kubwa katika neno la MUNGU bibilia inasema katika (MITHALI 12:18) kuna anenaye bila kufikili, kama kuchoma kwa upanga bali ulimi wa mwenye haki ni afya

Matatizo mengi uliyo nayo katika maisha yako, ndoa, biashala,kazini, shambani, na katika jamii anayo kuzunguka. yanasababishwa na matumizi mabaya ya usemi wako unawakwaza watu kwa usemi wako,

(MITHALI 10;19) katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu baliu yeye azuiaye midomo yake hufanya akili, tunza mdomo wako kwa usalama wako mwenyewe, Wasifu wa mtu sio mavazi tu bali hutemea maneno ya kinywa chako mwenyewe

Mpumbavu na mwenye hekima wakinyamaza huwezi kuwatambua mpumbavu ni yupi na mwenye hekima ni yupi, utawatambua tu wakianza kujieleza ndipo atajulikana mpumbavu na mwenye hekima, jitaidi sana kufikili kabla haujasema usije ukaonekana mpumbavu machoni pa watu,

hiki ndicho kipimo cha utu wako na heshima yako mbele ya wanao kutazama, ni aibu kwa mtu mwenye utashi na ukwasi kutamka hadhalani maneno yasiyo faa mbele ya jamii

BWANA YESU AKUBALIKI
 NI WAKATI WA KUMUABUDU BABA                                                                                                                                                                                    Katika kitabu cha (YOHANA MTAKATIFU 4:23).                                                                                    Neno linasema kuwa,  lakini saa inakuja nayo sasa ipo. Ambayo waabuduo halisi wata mwabudu baba katika ROHO na kweli. kwamaana baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                  Waabuduo halisi niwale wanao mwabudu MUNGU BABA katika ROHO na kweli, wapendwa kimefika kipindi cha kuacha utani na maswala ya ibada. kwakua mwisho umekaribia sanaa. ibada yoyote inayo fanywa  bila uwepo wa ROHO MTAKATIFU ni ibada ya sanamu. Ibada ya namna hiyo hutaona uwepo wa MUNGU bali ni maigizo  katika ibada kwa sababu ya mapokeo ya wanadamu                                                                                                                                                                                                         katika (1KORITHO3:10) Neno linasema  kwa kadri ya nehema ya MUNGU niliopewa mimi kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima naliweka msingi na mtu mwingine anajenga juu yake. lakini  kila mtu na angalie jinsi anvyojenga juu yake.                                                                                                                                                                                   katika ibada unayo mpa MUNGU kila siku , angalia je unayafanya yalio mapeznzi ya MUNGU? au nimatakwa ya wanadamu. kila mtu atatowa hesabu ya ibada yake mbele za BWANA.                                                                                                                                                                                   (1KORITHO3:11) neno linasema maana msingi mwingine hakuna mtu awezae kuuweka. isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa  yani YESU KRISTO.nikwalike unapo fanya ibada manisha kwamaana zamani hizi nizauovu .Watu wanautukuza ushetani kuliko MUNGU,watu wanautukuza ufreemason,kuliko YESU BWANA wanatukuza pepo kuliko RO
HO MTAKATIFU ,wanatukuza kuzimu kuliko mbinguni                                                          

(2KORITHO3:17) basi BWANA ndiye ROHO walakini alipo ROHO WA BWANA hapondipo penye uhuru mluhusu ROHO WA BWANA atawale maisha yako ili upate uhuru kamili. Kamwehautautukuza ushetani maishani mwako 

(2KORITHO3;16) Lakini wakati wowote utakapo mgeukia BWANA ule utaji wa kutuza ushetani utaondolewa. Upoutaji ulio kufunika.ndiyo maana unauona ushetani kuliko MUNGU na wakati huwo unasahau kuwa MUNGU NI MKUU zidi ya shetani. shetani sii kitu mbele zake.

                                                                                                                                                                              
Vipo vitu vingi vinavyoleta utaji katika maisha yako ya rohoni.
 Unashindwa kuona mbali 1. Inaweza ikawa ukoo wako.2 Dini za mababu na mapokeo ya dini, 3, Rafiki zako,4, Ekimu yako,5, Utajiri wako 6, Ndoa yako nk hivyo vyote vinaweza vikawa utaji katika maisha yako ukawa kipofu ,ukashidwa kumuona MUNGU.  ROHO WA MUNGU akusaidie ,macho yako yafunguke. ukamuone MUNGU maishani mwako wala sio shetani.
    Ndugu somo hili lina mapana sana kwaushauri zaidi wasiliana nami kwakutumia number hii +255 759 893 359 au +255 787 410 346
 BWANA WETU YESU AKUBARIKI

Bwana YESU asifiwe, Mbarikiwe na BWANA.
Naomba niitambulishe huduma hii kwenu, MUNGU amekuwa akitutumia katika viwango vikubwa sana. wagonjwa wamekuwa wakipona, waliofungwa na nguvu za giza wamekuwa wakiwekwa huru, na watu wamekuwa wakishudia matendo makuu ya MUNGU kutokana na huduma hii.
Unakaribishwa wewe, mwambie na mwingine kwenye muujiza wako.

MAWASILIANO
PIGA NAMBA +255 759893359  au +255 787410346
P.O.BOX 1466 MBEYA-TANZANIA

Nawakaribisha kutembelea ukurasa huu mara kwa mara kwaajiri ya kujifunza zaidi neno la MUNGU,
*****************************MUBARIKIWE************************

KUJITANGAZIA UHURU
Kujitangazia uhuru kutoka katika utumwa wa kiroho, kuwatangazia nduguzako uhuru kutoka katika utumwa wa kiroho ni kazi inayohitaji kusimama kwako mwenyewe na kujitambua.
Ezekiel 37:3    BWANA MUNGU alimwambia Ezekieli "Mwanadamu, je mifupa hii yaweza kuishi?"  Ezekiel akamjibu "BWANA MUNGU wajua wewe"

 Ezekiel 37:4  akamwambia "Toa unabii juu ya mifupa hii uiambie enyi mifupa mikavu lisikie neno la  BWANA"

Ezekiel 37:5  BWANA MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya "Tazama nitatia pumzi ndani yenu nanyi  mutaishi.

Kama BWANA MUNGU alivyomwambia Ezekieli, na wewe ni Ezekieli wa familia yako, biashara yako, mashamba yako, ndoto zako na nchi yako. Tabiri kwa yale unayotaka yatokee ondoa ukaufu, tabiri uzima.
Ondoa kushindwa, tabiri ushindi ndipo utayaona mafanikio makubwa.

Ezekiel 37:11    Kisha akamwambia Ezekieli "Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli, tazama wao husema mifupa yetu imekauka, matumaini yetu yametupotea, tumekatiliwa mbali kabisa.

Ezekieli 37:12-13  BWANA MUNGU akamwambia ezekieli "Basi tabiri uwaambie BWANA MUNGU asema hivi, tazama nitafunua makaburi yenu na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu enyi watu wangu, nami nitawaingiza katika nchi yenu.
 
Kuna ushindi baada ya kuwekwa huru, kuna kutawala baada ya kuwekwa huru, kuna umiliki baada ya kuwekwa huru, kuna amani baada ya kuwekwa huru.
Chukua hatua leo ukajitangazie uhuru wako na ubarikiwe na BWANA kwa kujitangazia uhuru wako.